Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Na Mwandishi Wetu-GPL
MKUU wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amefafanua mpango wa mamlaka
yake katika kuliendeleza Jiji la Dar es Salaam ili kuleta ufanisi,
maendeleo na usalama kwa wakazi wake.
Makonda
ameyasema hayo leo katika mahojiano na kituo cha radio cha Clouds FM cha
jijini wakati wa kipindi kijulikanancho kama Power Breakfast.
Miongoni
mwa mambo aliyoyalenga ni pamoja na kusisitiza watu kufanya kazi, kupiga
vita uvutaji wa shisha, ushoga, na kuendeleza miundombinu mbalimbali
kwa ajili ya huduma za wakazi wa jiji hilo.
Kuhusu
usalama, kiongozi huyo alisema mamlaka ya mkoa yatafanya ukaguzi katika
sehemu yoyote jijini kwa ajili ya kuhakikisha usalama na ulinzi wa
wananchi, jambo ambalo alitaka lipewe ushirikiano na wakazi wote.
Akizungumzia
ajira, alisema kuna mpango wa kuwachukua vijana zaidi ya 1,200 ambapo
watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali ambao watapatikana kwa uchambuzi
maalum.
“Tuna
mkakati wa kuwachukua vijana zaidi ya 1,200 kwa ajili ya kuwapeleka
katika mafunzo ya ujasiriamali, lakini ni lazima tuwatambue kwanza watu
hao,” alisema.
Alidokeza
kuwa kuna mpango wa kupanua muda wa kufanya biashara jijini tangu
asubuhi hadi saa nne za usiku ili kuwapatia watu huduma kwa muda mrefu
na kwamba kilichotakiwa ni kuimarishwa kwa usalama ikiwa ni pamoja na
kuongeza taa sehemu mbalimbali za jiji.
Mambo
mengine aliyozungumzia ni dhamira ya kuwawezesha walimu wa mkoani kwake
waanze kusafiri bure katika mabasi ya mwendo kasi na kutowapa pesa
ombaomba mitaani ili kuwafanya waondoke jijini.
Kuhusu
maovu mbalimbali yanayofanyika jijini, Makonda alishutumu ushoga,
utapeli na uvutaji wa madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na shisha.
“Ushoga
umepingwa na vitabu vya dini na hakuna sheria inayoruhusu ushoga, kwa
hili najua watu watanitukana sana lakini nguvu niliyo nayo hakuna wa
kunisimamisha,” alisisitiza huku akiwaonya watu wanaojiingiza katika
utapeli kwa kutumia majina ya watu wengine, likiwemo jina lake |
July 19, 2016
RC MAKONDA AFAFANUA MPANGO WA KUIENDELEZA DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment