Kama ulipata nafasi ya kutizama mchezo wa Jumamosi kati ya Manchester United na mabingwa watetezi wa kombe la EPL, Leicester City basi ni wazi utakuwa unajua kuwa nahodha wa Man United, Wayne Rooney alianzia benchi katika mchezo huo na kuingia kipindi cha pili dk. 83, mchezo ambao ulimalizika kwa United kuibuka na ushindi wa goli 4-1.
Baada ya mchezo kumalizika kocha wa Man United, Jose Mourinho alikutana na maswali ya waandishi wa habari wakitaka kujua sababu ya Rooney kuanzia benchi na Mourinho kusema sababu ya Rooney kuanzia benchi ni kutaka kuwa na washambuliaji wawili wenye kasi na Mata kucheza nafasi yake hivyo ikabidi Rooney kusubiri nje.
“Nahodha wangu ni nahodha wangu tu, kama akiwa uwanjani au akiwa nyumbani ni nahodha wangu, kwahiyo hilo sio tatizo. Katika kikosi chetu dhidi ya Leicester tuliona suluhisho la kupambana nao ni kuwa na watu wawili wenye kasi na Mata akacheza nafasi ambayo alitakiwa kucheza’
“Ni mchezaji wangu [Rooney], namwamini na ana furaha kama niliyonayo mimi muda huu na kwa timu,” alisema Mourinho.