Mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Stand United iliyokuwa mwenyeji wa
Yanga, umemalizika kwa mabingwa watetezi wa VPL, Yanga kukubali kichapo
kutoka kwa chama la wana, Stand United.
Mchezo
huo umemalizika kwa Yanga kufungwa goli moja kwa bila, goli likifungwa
na Pastory Athanas katika dakika ya 58 baada ya mabeki wa Yanga
kuchanganyana na Athanas kutumia nafasi hiyo kwenda kufunga goli
lililodumu hadi mchezo unamalizika.
Kwa matokeo hayo, Stand United imefikisha alama 12 ikiwa nafasi ya tatu ya msimamo wa VPL na Yanga ikisalia na alama 10.
Kipigo
hicho kwa Yanga kinakuja ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kukutana na
watani zao wa jadi Simba, mchezo unaotaraji kupigwa Jumamosi ya Oktoba
mosi katika dimba la taifa
No comments:
Post a Comment