Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya
Maweni ya Mkoa wa Kigoma na kujionea mambo mbalimbali.
Katika
ziara hiyo, Naibu Waziri aliweza kubaini mapungufu kadhaa ambapo
amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatatua matatizo hayo
haraka. Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na kutokuwa na mfumo maalum
wa kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ili kudhibiti mapato huku
akiwataka ndani ya miezi mitatu wawe wameshakamilisha mfumo huo.
Mbali
na hilo pia amewataka kuzingatia utunzaji wa vifaa vya Maabara ya
Hospitali hiyo kwani licha ya kuwa na jingo zuri lakini bado hali ya
utunzaji imekuwa ndogo na hata kusababisha vifaa vingine havifanyi kazi.
Kwa
upande wa Chumba cha upasuaji (Theatre) amewaagiza kuhakikisha
wanaondoa kasoro zote muhimu kwani Chumba hicho kimekosa sifa ya kuitwa
Chumba cha Upasuaji cha Hospitali ya Mkoa wa Kigoma baada ya kushuhudia
ufinyu wa jengo lenyewe, ukosefu wa vifaa na hali nzima ya sehemu ya
utendeaji kazi.
Naibu
Waziri wa Afya ametembelea Mkoa Kigoma katika ziara yake ya siku mbili,
awali aliweza kutembelea Kituo cha Afya cha Uvinza kilichopo Wilaya ya
Uvinza, pamoja na Hospitali ya Heri Mission iliyopo Wilayani Buhigwa
Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokelewa na madaktari waandamizi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, wakati wa kuwasili Hospitalini hapo kwa ziara ya kikazi mapema jana Septemba 29.2016. |
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Kigoma |
No comments:
Post a Comment