Na Barnabas Lugwisha |
Mvutano huo baina ya vigogo hao umesababisha hatimaye Lipumba kuvuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka Katiba ya CUF wakati huo huo Lipumba akisema kikao kilichofanyika Zanzibar na kumvua uanachama si halali.
Vuta ni kuvute hiyo imesababisha mpasuko ndani ya CUF. Jana Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif alisema atatinga ofisini hapo leo asubuhi pamoja na timu yake kuendelea na kazi za chama , upande mwingine Lipumba akimwita Maalim Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni ili ampangine kazi nyingine, ni matumani yangu kuwa vyombo vya dola vitaingilia mgogoro huo hasa wa ujio Seif na timu yake ili kusiwepo umwagaji wa damu leo pale Buguruni.
Viongozi hao wawili watambue kwamba hakuna amani wala maridhiano yatakayopatikana nje ya meza ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment