Baaya
ya kuahirishwa ile kitu inaitwa UKUTA tarehe moja mwezi huu kuna dalili
tena ya kuahirishwa tena kesho, kitu hiyo ilipangwa ifanyike kesho
kesho . Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuahirishwa kwa
Ukuta hadi tarehe mosi Oktoba. Serikali ilipiga marufuku kufanyika kwa Ukuta na kwamba atakayejaribu atakiona kile kichomnyoa kanga manyoya. Wiki iliyopita Salum Mwalimu, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, alipoulizwa na MwanaHALISI Online kuhusu uzinduzi wa operesheni hiyo hasa ikizingatiwa kuwa zimebaki siku chache kabla ya Oktoba Mosi, alijibu kuwa, “Ukuta siyo tarehe.” “Ukuta ni fikra zinazoishi ndani ya mioyo ya watu na zitaendelea kuishi. Suala siyo kubaki kwa siku tano au kumi. Tunasubiri tupate mrejesho kutoka kwa viongozi wa dini halafu tutafanya uamuzi juu ya suala hilo,” alisema. Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, ametoa taarifa jioni ya leo akisema, chama hicho kitatoa tamko juu ya suala hilo siku ya kesho. “Taarifa rasmi kuhusu Ukuta na hatima ya siku ya maandamano na mikutano nchi nzima iliyotangazwa na chama, itatolewa kesho Ijumaa, Septemba 30, 2016, saa 5:00 asubuhi, mzungumzaji mkuu atakuwa ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama Taifa,” amesema Makene. Dalili za awali zinaonyesha kuwa, Chadema inaweza kuahirisha tena kufanyika kwa uzinduzi wa operesheni hiyo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kuchelewa kupata majibu ya viongozi wa dini juu ya jaribio lao la kuonana na Rais John Magufuli ili kutafuta suluhu. Taarifa zaidi zinadai kuwa, mpaka sasa jaribio la viongozi wa dini kuonana na Rais Magufuli na kujadili suala la kuruhusu kufanyika kwa mikutano na maandamano nchi nzima limegonga mwamba. |
September 30, 2016
UKUTA WA UKAWA KUAHIRISHWA TENA LEO?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment