![]() |
Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL) inaendelea leo Septemba 30, 2016 kwa mchezo mmoja
tu, unaozikutanisha timu za Toto Africans na Ndanda ya Mtwara katika
mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kama ilivyo kwa leo,
kesho pia kutakuwa na mchezo mmoja tu utakaowakutanisha watani wa jadi,
Young Africans na Simba katika dimba la Taifa, Dar es Salaam. Mchezo
huo, umekuwa na hamasa ya aina yake.
Lakini kwa siku ya
Jumapili, michezo itakuwa mitano ambako Mbeya City itaikaribisha Mwadui
kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itakuwa mwenyeji wa
Stand United kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon
itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani
Morogoro.
Mbao baada ya kucheza na
Ruvu Shooting wiki iliyopita, ilibakia Mlandizi mkoani Pwani kusubiri
kucheza na JKT Ruvu Jumapili kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi
wakati Kagera itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba mkoani Kagera.
|
September 30, 2016
LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA WIKIENDI HII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment