TAASISI 10 ZA SERIKALI ZIMEFANYA CHINI YA KIWANGO YA SHERIA YA MANNUZI YA PPRA.
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga akizungumza na
waandishi wa habari juu ya ukaguzi waliofanya katika taasisi za serikali
katika kufuata sheria ya manunuzi leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga jijini Dar es Salaam leo.
Na Yassir Adamu, Globu ya Jamii.
RIPOTI
ya Ukaguzi kwenye manunuzi ya umma ya mwaka wa fedha 2015/2016
uliofanywa na mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) unaonyesha
taasisi 10 nunuzi zimefanya manunuzi chini ya kiwango
kisichoridhisha chini ya asimia 60.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya
PPRA, Balozi Matern Lumbanga amesema taasisi hizo zimefanya chini ya
kiwango katika kufanya manunuzi yake kwa mujibu wa sharia ya
manunuzi.
Amesema jumla
ya PPRA imefanya jumla ya mikataba 21,313 ya manunuzi yenye thamani ya
sh.Trioni 1.05 katika ujenzi ,vifaa, huduma ushauri wa kitaalam .huduma
zilizohitaji mikatba ya ushauri wenye thamani ndogo pamoja na mikataba
yenye makubaliano maalum.
Balozi
Lumbanga amezitaja taasisi zilizofanya chini ya kiwango ambazo ni
Taasisi ya Uzalishajin (NIP), Dar es Salaam Rapid Transist (DART),
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Makumbusho ya Taifa, Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kampuni ya
Reli Tanzania (TRL), Taasisi ya Mifupa (MOI), Halmashauri ya Manispaa ya
Msoma pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Bukoba (Buwasa).
Amesema
mikataba 122 ya ukusanyaji wa mapato iliyokaguliwa kwenye mamlaka tisa
ya serikali za mitaa kwa mujibu wa mikataba iliyokaguliwa imebainika
kuwa na mapungufu kadhaa katika usimamizi wa mikataba hiyo na kufanya
halmashauri kushindwa kukusanya kiasi cha sh. Milioni 761.54.
Aidha
Balozi Lumbanga amesema kuwa kushindwa kukusanya mapato hayo
Halmashauri zimesababisha hasara halmashauri hizo zimeshindwa kuchukua
hatua zozote dhidi ya wazabuni waliopewa miradi kutokana mikataba
walioingia.
No comments:
Post a Comment