Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti
WAZIRI
mkuu Kassim Majaliwa,amesema mpango wa kutoa mil.50 vijijini ambao
ulioahidiwa na serikali,unatarajiwa kuanza mwakani baada ya kupitisha
bajeti ya fedha 2017-2018.
Aidha
amewatahadhalisha wananchi wasidanganywe na kutapeliwa na baadhi ya
watu wanaotaka kujipatia fedha wakiwashawishi waunde vikundi kisha
kuwachangisha fedha za usajili wa vikundi hivyo.
Majaliwa
ameeleza kuwa mpango huo ukiwa tayari serikali itatangaza rasmi na
kutoa taarifa kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa,wilaya na
wabunge ili waweze kutaarifu watu kwenye maeneo yao.
Ameeleza
mpango huo, upo pale pale ambapo fedha hizo zitatengwa kwa ajili ya
kuwezesha makundi ya vijana,wanawake na mengine kwa lengo la kuwainua
kiuchumi.
Waziri
mkuu aliyasema hayo ,wilayani Kibiti,baada ya mbunge wa jimbo hilo Ally
Ung’ando kutoa kueleza kero inayowakabili vijana kukosa ajira na
kusuasua kwa kiwanda cha samaki ambacho hakifanyikazi.
Hata
hivyo alieleza kuwa bunge lijalo ndilo litatangaza fedha zitakazotengwa
kwa ajili ya mpango huo pamoja na utaratibu utakaotakiwa kufutwa
utatangazwa katika kipindi hicho.
Majaliwa alisema fedha hizo zitasaidia kukopesha makundi mbalimbali yaliyopo kwenye vijiji ili kuzalisha na kuinua biashara zao.
“Mkisikia
mtu anakuja kuwaambia suala la mil.50 leo huyo ni tapeli,mpango huo
bado,tutakapokuwa tayari mbunge atapata taarifa na kuwaambia na serikali
itaeleza mpango huo ukianza.”
“Fedha
hizo sio za kugawa na fedha hizi hazijaanza na ninaeleza kutaarifa
kuna matapeli wanaanza kuwadangaya unda vikundi unda vikundi ,na baada
ya hapo wakitakamchangie 10,000 kwa watu 30 ama 40 na kujipatia
fedha,kuweni macho”alisema Majaliwa.
Akizungumzia
kuhusu viwanda alivitaka vijengwe na vifanyekazi ili kutoa wigo mkubwa
wa ajira ndani ya jamii ikiwemo vijana ambao wanatangatanga kusaka
ajira.
Majaliwa
alisema kuchelewa kufanya kazi kwa kiwanda cha samaki na kiwanda cha
kuchakata muhogo vilivyopo Kibiti,atakutana nao ,ili wamueleze
walipokwama na kutafuta ufumbuzi.
Alieleza
lengo la serikali ni kuinua sekta ya viwanda kwa kushirikiana na
kukaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza kwenye viwanda kwa
malengo makuu matatu
Majaliwa
alisema viwanda vingi vikijengwa vitasaidia kuongeza wigo wa ajira
nchini,kuinua uchumi na kuuza mazao mbalimbali yanayolimwa na
kuyaongezea thamani kuliko kuuza mmoja mmoja mashambani.
Alisema
atakaa na kufuatilia tatizo linalowakwamisha wenye kiwanda cha samaki
na cha kuchakata muhogo vilivopo wilayani hapo ili kutafuta ufumbuzi na
vifanye kazi kwa maslahi ya jamii.
Awali
mbunge wa jimbo la Kibiti ,Ally Ung’ando ,alimwambia wziri mkuu kuwa
kuna changamoto ya fedha za vijana na wanawake kutotolewa kwa wakati .
Alitaja
kero nyingine kuwa ni tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hao na
kukosa mikopo na mitaji suala linalosababisha vijana wengi kushindwa
kufanya ujasiliamali.
Ung’ando
alisema huwa akikaa na baadhi ya vijana na kuwashauri wajiunge vikundi
jambo litakalowawezesha kusaidiwa kirahisi na taasisi mbalimbali
na halmashauri kuliko kujiweka mtu mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment