Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad
Masauni akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika
mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya
kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo
ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu
Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo
unafanyika leo katika Ukumbi wa wa Mikutano wa Kanisa Katoliki, Jimbo la
Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa
Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa
makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo
pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala
mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo
unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga akitoa
taarifa ya matukio mbalimbali ya ajali za barabarani nchini katika
mkutano wa Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini. Mkutano huo
ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani
nchini. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni, na kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry
Bantu. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa wa Mikutano wa Kanisa
Katoliki, Jimbo la Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
No comments:
Post a Comment