Waziri mkuu wa zamani wa Israel aliyewahi kuhudumu pia kama rais Shimon Peres amefariki dunia akiwa na miaka 93.
Aliugua kiharusi wiki mbili zilizopita na hali yake ikawa mbaya zaidi ghafla Jumanne.
Bw
Peres, ambaye alikuwa mmoja wa waliosalia kutoka kwenye kizazi cha
wanasiasa waliokuwepo wakati wa kuundwa kwa taifa la Israel mwaka 1948,
alihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo mara mbili na mara moja kama
rais.
Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1994 kwa mchango wake
katika mashauriano yaliyopelekea kutiwa saini kwa mkataba wa amani kati
ya Israel na Palestina mwaka mmoja awali.
Wakati mmoja, aliwahi
kusema kwamba Wapalestina ndio "majirani wa karibu zaidi" wa Waisraeli
na wanaweza kuwa "marafiki wa karibu zaidi".
Bw Peres amefariki
akitibiwa katika hospitali moja iliyopo karibu na mji wa Tel Aviv mapema
Jumatano, jamaa zake wa karibu wakiwa karibu naye.
Alikuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Sheba Medical Centre baada ya kupatwa na kiharusi 13 Septemba.
Rais
wa Marekani Barack Obama amemweleza Bw Peres kama "rafiki wa karibu"
kwenye taarifa, na akasema: "Aliongozwa na maono ya heshima na utu na
alifahamu kwamba watu wenye nia njema wanaweza kustawi pamoja."
Bw
Peres alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa pamoja na Waziri Mkuu
Yitzhak Rabin, ambaye baadaye aliuawa, na Kiongozi wa Wapalestina Yasser
Arafat.
|
September 28, 2016
PUMZIKA KWA AMANI MZEE SHIMON PERES
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment