Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI
imetenga tilioni moja ,kwa ajili ya kumaliza vijiji 8,000 nchini
ambavyo havijafikiwa na huduma ya nishati ya umeme kupitia mradi wa
umeme vijijini(REA).
Imesema
washatangaza zabuni na kwasasa tayari wakandarasi wameshapatikana na
kupewa wilaya za kuzifanyia kazi ikiwemo vijiji vilivyokuwa havijafikiwa
na umeme wilayani Kibiti.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa,alisema hayo wakati akizungumza na wananchi stand ya Kibiti ,Bungu na Nyamisati wilayani Kibiti.
Alisema
nyaya,nguzo inaweka serikali hivyo wananchi wa Kibiti wajipange kulipia
gharama za kupata umeme ambapo kwa sasa ni sh.27,000 kutoka 450,000 za
awali.
“Umeme
huo utapelekwa hadi nyumba za makuti,hiyo hakuna sababu ya kuilalamikia
serika kukosa umeme,kikubwa ni kujiandaa kulipia gharama hizo”
“Anzisheni
miradi ya kufuga kuku majumbani,ambao wanazaa wenyewe na mkija kuuza ni
10,000 kuku mmoja,hivyo ni kuku watatu tuu,jamani hiyo nayo
itawashinda,acheni kulalamika lalamika,kulia lia hamna hela hata kufuga
kuku kutawashinda”aliwashauri Majaliwa.
Majaliwa alieleza kuwa kwa kusogezwa kwa huduma ya umeme vijijini itasaidia kuvutia wawekezaji na kuinua maendeleo .
Alisema wanamalizia maeneo na vitongoji vyote vilivyo mbali na mtandao wa umeme na wanataka umeme uende kwa kila mwananchi.
Aliwataka
wananchi hao kukimbilia huduma hiyo maraitakapofikishwa kwenye maeneo
yao ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya maeneo yao na kuondokana na
hali ya sasa ya kuishi kwa kutegemea koroboi na taa za kuchaji.
Alisema
awali kulikuwa na vijiji vingi visivyo na umeme lakini kwa sasa vijiji
katika maeneo mengi vimeshapata nishati hiyo na kubakia 8,000 ambavyo
katika awamu hii vinatarajiwa kukamilishwa vyote.
Majaliwa
alisema huduma hiyo ni muhimu kwani mbali ya kutumiwa majumbani lakini
pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha
zahanati,shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.
Awali
uongozi wa chama cha mapinduzi (CCM),wilayani hapo,ulisema umeme bado
haujafika katika km 7 pekee ,kutoka Jaribu mpakani hadi ulipoishia
umeme.
No comments:
Post a Comment