Rais wa Chama cha wafamasia
Tanzania (PST) Ndg. Michael Kishiwa (aliyesimama)akitoa taarifa ya Chama
kwa kifupi kwa Mgeni Rasmi Mhe. Mrisho Gambo katika Kongamano la 49 la
wafamasia Tanzania linalofanyika Jijini Arusha
Wanachama wa PST wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo akitoa hotuba katika ufunguzi wa kongamano la 49 la
Chama cha Wafamasia Tanzania
Wajumbe wa kongamano wakiendelea kufuatilia Hotuba ya Ufunguzi
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho
Gambo(Kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa
Hiti Silo katika Kongamano la wafamasia linalofanyika katika Jiji la
Arusha.
……………………………………………………………………….
Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA
SERIKALI imesema kuwa inaanza
kufanya maboresho kwa kuandaa na kuhakikisha Sera ya Uboreshaji wa
Viwanda vya Dawa vilivyopo nchini kwa kuwawezesha na kuwajengea uwezo
wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha dawa na kupunguza uagizaji wa
dawa kutoka nje ya nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo kwa niaba ya Waziri wa
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alipokuwa
akizungumza katika Kongamano la 49 la Chama Cha Wafamasia Tanzania
(PST),linalofanyika jijini hapa kwa siku mbili.
Akizungumza kwa niaba ya Mhagama,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,alisema kuwa kutokana na umuhimu wa
sekta hiyo ya dawa, Serikali inaangalia taaluma hiyo kwa macho mawili
kwa lengo la kuiboresha ili iweze kutoa huduma bora.
“Wizara yangu inaangalia taaluma
hii kwa macho mawili katika kuhakikisha kuwa sekta ya dawa inaboreka na
inakua na hatimaye kuweza kukuza uchumi wetu, kwa kuwawezesha na
kuwajengea uwezo wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha zaidi ikiwa
ni pamoja na kuwahakikishia soko ndani ya nchi na kupunguza uagizaji wa
dawa kutoka nje ya nchi na hivyo kuwa na dawa bora, salama na zenye
ufanisi”
“Endapo tutazalisha dawa zetu
wenyewe hii itatupunguzia gharama zisizo za lazima kuagiza dawa nje ya
nchi, sambamba na hili pia tunaboresha vyuo vya Wafamasia ili waweze
kutoka wataalamu bora wa masuala haya ya madawa,”alisema Gambo
Akizungumzia suala la wizi wa
dawa katika hospitali za serikali,alisema kuwa Serikali haina mchezo na
yoyote atakayokiuka maadili ya taaluma hiyo na kuwa watawachukulia hatua
kali za kisheria ili wananchi wapate huduma bora za dawa.
“Mbali na changamoto ya upungufu
wa dawa, wafanyakazi wasio waadilifu ambao wanatumia nafasi zao vibaya
wanashirikiana na baadhi ya wafanyabiashara na kuuza dawa, hili ni
suala muhimu PST jadilianeni suala la maadili kwani hatua za kisheria
dhidi yao zitachukuliwa”alisema
Awali Rais wa PST, Michael
Kishiwa, aliiomba Serikali kuongeza udahili wa wanafunzi wa famasia
wakiwemo mafamasia wasaidizi ili kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa.
Alisema hivi sasa idadi ya
watanzania ni kubwa, lakini wataalamu wa dawa Wafamasia ni 1,200, hali
inayochangia kuwepo kwa watoa huduma hiyo wasio na sifa.
Alisema kutokana na kukosekana
wanataaluma kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi yao kukiuka maadili
na wengine kufanya kazi ya utoaji dawa pasipokuwa na uelewa nayo, hali
ambayo hatari kwa afya za binadamu
No comments:
Post a Comment