Jeshi
la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu watatu kwa kosa la kughushi
nyaraka za ofisi na kupelekea wizi wa jumla ya kiasi cha sh,50 milioni
mali ya chama cha wakulima cha Tanganyika(TFA).
Kushikiliwa kwa watuhumiwa hao kunakuja zikiwa ni siku chache tu baada ya jeshi hilo kumshikilia
na kisha kumwachia kwa dhamana aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya muda wa
TFA ,Meynard Swai kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali na fedha ndani ya
chama hicho.
Mwenyekiti
huyo alishikiliwa kwa siku kadhaa na jeshi la polisi mkoani hapa mwezi
uliopita jijini na kisha kuhojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana ambapo
kwa sasa polisi bado wanaendelea na uchunguzi dhidi ya mashtaka
yanayomkabili.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Arusha,Charles Mkumbo alisema kwamba watuhumiwa hao walishikiliwa
katika maeneo tofauti hapa nchini.
Aliwataja
kwa majina walioshikiliwa kuwa ni Salvatory Mwandu,Simon Mwandu pamoja
na mkazi wa jijini Dar es salaam,Jesca Canisius ambao kwa sasa
wameachiwa kwa dhamana.
Mkumbo,alisema
kwamba watuhumiwa hao wako chini ya uchunguzi na jeshi lake na bado
linaendelea na upelelezi wa kina huku akisisitiza ya kwamba hawatasita
kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote atakayevunja sheria za nchi.
No comments:
Post a Comment