Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 220 jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 80 kutoka kwa
Balozi wa Pakistan nchini, Amir Khan (wapili kushoto ukiwa ni mchango
kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Makabidhiano
hayo yalifanyika kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam
Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na kulia ni Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa
Mwakilishi Mkazi wa Tasisi ya Aga khan nchini, Amin Kurji (kulia) ukiwa
ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na wapili kulia ni
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Baadhi
ya watu walioshiki katika tukio la kukabidhi jumla ya shilingi 190
ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera
kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa
China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alipozungumza baada ya kupokea mchngo huo kwenye hoteli
ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. milioni 190 kutoka kwa
balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa China Mhe. Gou
Haodong na Taasisi ya Aga Khan.
Fedha
hizo zimetolewa ili kusaidiia wananchi walioathirika na tetemeko la
ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na
kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.
Pia
tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081
zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata
uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
Makabidhiano
ya michango hiyo, yamefanyika leo (Ijumaa, Septemba 30, 2016) kwenye
Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri Mkuu
aliwashukuru kwa michango hiyo na alitumia fursa hiyo kuwaomba wale
walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi zao.
“Ninawaomba
wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi kwa kuzileta ofisini
kwangu au kutuma kupitia akaunti ya maafa iliyofunguliwa katika Benki ya
CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA –
Swiftcode: CORUtztz,” amesema.
Amesema
watu walio mbali na benki watumie namba za simu zilizotolewa mahsusi
kwa ajili ya kupokea michango ya maafa hayo ambazo ni 0768-196-669
(M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).
Akikabidhi
hundi kwa Waziri Mkuu, Balozi wa Pakistan, Mhe. Amir alisema wanaamini
mchango huo wa sh. milioni 80 walioutoa utasaidia kuwapunguzia uchungu
wananchi wa Kagera kutokana na athari zilizosababishwa na tetemeko la
ardhi.
Kwa
upande wake Kaimu Balozi wa China Mhe. Haodong alimweleza Waziri Mkuu
kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari walishawapeleka madaktari na
wataalamu wengine mkoani Kagera na leo walikuwa wanakamilisha ahadi yao
ya kutoa mchango wa sh. milioni 60.
Naye
Muwakilishi Mkazi wa Taasisi za Aga Khan nchini, Amin Kurji alimkabidhi
Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 50.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, SEPTEMBA 30, 2016
No comments:
Post a Comment