Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.
Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo.
Pia Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.
Vile vile serikali yake iko katika hatua za ujenzi wa daraja la kisasa litakalo anzia maeneo ya daraja la Sarenda litakalo pitia baharini.
Hadi sasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inaendelea nchi nzima ikiwemo mradi wa barabara za juu (Flyover) maeneo ya Tazara.
Aidha, Dk. Magufuli amesema serikali yake iko katika hatua za kutengeneza na kuboresha miji yake ili iwe ya kisasa.