KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 29, 2016

VODACOM YAZITAKIA KILA LA KHERI SIMBA NA YANGA

Image result for vodacom
Akiongea na mtandao huu kwa niaba ya Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamni wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella, amesema wakiwa kama wadhamini wakuu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara,Wanazitakia kila la kheri timu ya Yanga na Simba katika mzunguko wa kwanza kwa timu hizi kubwa hapa nyumbani  zitakazomenyana siku ya jumamosi ya tarehe 1 mwezi Oktoba katika uwanja wa Taifa jijini Da res Salaam. Na kuamini kwamba mchezo huo utakuwa mzuri na wakuburudisha washabiki wote wa timu hizi watakaofika uwanjani kuushuhudia kwani ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana tangia msimu huu kuanza,Pia napenda kuwatoa wasiwasi wapenzi wa mchezo huu ambao hawatapata na nafasi ya kufika uwanjani kwani Vodacom Tanzania haitawaacha mbali na matokeo yatakayokuwa yakiendelea uwanjani hapo”LIVE” ili kupata matokeo ya mchezo huo ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kujiunga na kifurushi cha ‘Soka bando’ na utakuwa unapata frusa ya kupata matokeo kiurahisi kabisa popote pale ulipo ya timu yako uipendayo kati ya Simba na Yanga.Kifurushi hichi ni chenye gharama nafuu ya shilingi 500/-ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa masaa 24.
Displaying 001.LIGI.jpg
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella
v Ili kununua kifurushi hiki anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga  namba *149 * 01#, Ofa mpya alafu chagua ‘Soka Bando’. Baada ya  hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga”  “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya  Mspoti.vodacom.co.tz

No comments:

Post a Comment