Mwamvua Mwinyi
WAZIRI
mkuu Kassim Majaliwa ,amesema serikali imewekeza kwa elimu ya mtoto wa
kike hivyo ataejitokeza kuvuruga katika harakati za elimu yo mtoto wa
kike atachukuliwa hatua kali za kisheria .
Aidha
amekemea utoro kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
na kutoa rai kwa wazazi na walezi kusimamia watoto wao ili waweze
kumaliza elimu.
Majaliwa
amesema kwa kutambua hilo ndio maana serikali imetenga sh.bil 21 kwa
ajili ya mpango wa elimu bure ambazo tayari wameshapeleka katika shule
za msingi na sekondari ili watoto waweze kupata fursa ya kusoma wakiwemo
watoto wa kike.
Akizungumzia
sekta ya elimu katika ziara yake mkoani Pwani,alisema mbali ya hayo
serikali inatarajia kuajili walimu 24,000 ambao watasambazwa katika
shule mbalimbali za msingi na sekondari na kuwaboreshea maslahi yao.
Alisema
tayari serikali imeagiza watoto wenye umri wa kupelekwa shuleni
wapelekwe na mzazi na mlezi ambae hapeleki mtoto shule atakamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Majaliwa aliitaka jamii pia kuhakikisha inapeleka watoto wao wenye miaka mitano kuwaanzisha shule za chekechea.
Alikataza utoro mashuleni na jamii isimamie hilo bila ajizi kwa lengo la kuinua taaluma kwa watoto kwa manufaa yao ya baadae.
“Msomeshe
watoto wote ikiwemo watoto wa kike,serikali imewekeza kwa watoto
wakike,bila kubughudhiwa na atakaebainika kumvuruga apelekwa jela,”
No comments:
Post a Comment