Dk. Mwele Malecela Mkurugenzi wa
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) akizungumza
na waandishi wa habari katika makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es
salaam wakati alipotangaza kongamano kubwa la watafiti litakalofanyika
tarehe 4 mpaka 6 Oktoba 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Dk. Mwele Malecela Mkurugenzi wa
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari wakati alipokuwa akizungumza nao leo,
Kulia ni Dk. Julius Massaga Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza
Utafiti/Mtafiti Mkuu wa NIMR.
………………………………………………………………………
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ilianzishwa kwa Sheria namba 23 ya mwaka
1979. Katika kipindi cha miaka 29 iliyopita Taasisi imekuwa ikiandaa
Kongamano la sayansi kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha watafiti,
watoa huduma za afya, watunga sera, wakufunzi, wahisani na wadau
wengine wa afya kuwasilisha na kujadili matokeo ya tafiti mbalimbali za
afya.
NIMR imeandaa Kongamano lake la
30 kuanzia tarehe 4 mpaka 6 Oktoba 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa
Kongamano hilo atakuwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Ufunguzi utakuwa saa 3 asubuhi
ya Oktoba 4, 2016.
Mada kuu ya Kongamano hilo ni
“Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya
dunia.” Jumla ya mada 220 zitawasilishwa na kujadiliwa katika Kongamano
hili la Siku 3. Mada hizo zitakuwa katika maeneo yafuatayo:
- Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana.
- Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake
- Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria
No comments:
Post a Comment