Waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
Waandishi wakiwa kwenye semina hiyo
Semina ikiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA
ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA), imewataka
Watanzania kuondoa hofu iliyojengeka kwenye jamii kuwa mifuko ya hifadhi
ya jamii ina hali mbaya kifedha.
Akizungumza
katika warsha maalum ya siku moja ya waandishi wa habari, iliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa SSRA, Ansgar Mushi alisema
kuwa mifuko hiyo haina hali mbaya kama wanavyodhani watu katika jamii
kwani ina fedha za kutosha.
“Watanzania
wamekuwa wakiambizana kuwa mifuko hii ina hali mbaya kifedha, napenda
kuwahakikishia kuwa ina fedha za kutosha kwani tumekuwa tukifanya
ukaguzi wa mara kwa mara. Katika kaguzi zetu za mara kwa mara hakuna
mfuko tuliobaini kuwa una kasoro au upungufu wowote,” alisema Mushi.
Aidha,
Mushi alisema kwa mwaka mifuko hiyo ya pensheni imekuwa ikikusanya
jumla ya sh trilioni 1.692 wakati mfuko wa bima ya afya (NHIF)
unakusanya sh bilioni 88.5 ambapo jumla ya makusanyo yote ni sh trilioni
1.78.
Kwa
upande wa fao la kujitoa, Mushi alisema licha ya kutawaliwa na
sintofahamu, fao hilo lilifutwa na Serikali kuanzia mwaka 2012 na kwa
sasa SSRA imeanzisha mchakato wa kuratibu uanzishwaji wa fao la upotevu
wa ajira.
Mushi
alisema kuwa fao hilo lilipofutwa, bado kulikuwa na mifuko iliyoendelea
kuruhusu kujitoa lakini kwa sasa wameamua waanzishe mchakato wa fao la
kupoteza ajira, ambalo ni mahususi kwa ajili ya kuwanufaisha waathirika.
“Fao
la Upotevu wa ajira litakuwa mahsusi kwa ajili ya wale waliopoteza
ajira zao, huku wakiwa wamechangia mifuko ya hifadhi kwa kipindi cha
miezi zaidi ya 18. Hawa watalipwa asilimia 33 ya mshahara wa mwisho kwa
kipindi cha miezi 6,”
“Kipindi
hicho cha miezi 6 kikiisha, mtu huyo kama hajapata ajira atawekwa
katika hatua nyingine ambapo ataruhusiwa kuchukua nusu ya fedha
alizochangia katika kipindi chake cha ajira,” alisema Mushi.
Akizungumzia
wale waliopoteza ajira zao wakiwa hawajafikisha kipindi cha miezi 18,
Mushi alisema kuwa wataruhusiwa kuchukua asilimia 100 ya fedha
walizochangia kipindi chote walipokuwa kwenye ajira.
“Watu
hao wataruhusiwa kuchukua fedha zao kwa asilimia 100 ambazo walichangia
kipindi wakiwa waajiriwa. Hata hivyo, napenda kuwaambia Watanzania
kuendelea kuichangia mifuko hiyo kwani ina manufaa zaidi nyakati za
uzeeni baada ya kustaafu,” alisema Mushi.
No comments:
Post a Comment