Ikiwa
imepita siku moja tangu ndege mbili mpya aina ya Bombardier Dash-8 Q400
za serikali kuzinduliwa kwa ajili ya kuanza safari zake rasmi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema safari za
ndege hizo zitasaidia kufufua hifadhi za utalii ambazo zilikuwa
hazifikiwi kutokana na kukosekana kwa njia rahisi ya kuunganisha safari
za watalii.
Waziri
Maghembe amezitaja mbuga, ardhi oevu na ghuba zitakazo fufuliwa kuwa ni
mbuga za Gombe na Katavi, ghuba za mahale na ardhi oevu ya Kirombelo,
ambazo kwa mujibu wa tafiti za kitalii zinaongoza kwa uzuri Afrika na
duniani kwa ujumla.
“Ndege
hizi zikianza safari zake mbuga nyingi zitafunguka ambazo awali
zilikuwa hazifikiwi na watalii kutokana na kutokuwepo usafiri wa
uhakika, ” amesema.
Amesema sababu nyengine iliyopelekea vivutio hivyo kutofikiwa na watalii ni gharama kubwa za usafiri.
“Hivi
sasa watalii katika baadhi ya maeneo wanatumia dola 1800 kusafiri yaani
kwenda na kurudi, mfano kutoka Kilimanjaro kwenda Kigoma watalii
wanalipa gharama ya usafiri 1600 kwenda na kurudi hii ni sawa na milioni
4 za kitanzania. lakini kwa sasa watalipa dola 150 pekee, ” amesema.
Maghembe
amesema ndege za ATCL zitakapoanza kazi zitasaidia kusafirisha watalii
wanaokwenda Zanzibar kwenda katika hifadhi nyingine zilizopo bara kama
Serengeti na Manyara kwa sababu utakuwepo usafiri wa uhakika na wa
gharama nafuu.
Ametaja hifadhi nyengine itakayonufaika na usafiri wa ATCL ni hifadhi ya bahari ya Marine Park ambayo ni ya 3 kwa ubora duniani.
“Mafia
kuna hifadhi ya bahari ilitengenezwa inaitwa Marine Park ni ya tatu kwa
ubora duniani lakini ilikuwa haifikiwi na watalii kwa sababu ya
kukosekana kwa usafiri wa uhakika, ila kwa ndege hizi kila mtalii
atatumia dola 100 kwenda na kurudi,” amesema.
Na Regina Mkonde
|
September 29, 2016
WAZIRI MAGEMBE ASEMA NDEGE MPYA ZITAPIGA JEKI UTALII NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment