BAADA
ya Profesa Ibrahim Lipumba (Pichani) kudaiwa kutimuliwa uanachama wa
CUF na yeye amejibu mapigo kwa kumwita Dar es Salaam Katibu Mkuu wa CUF
Seif Sharif Hamad ili ampangie kazi nyingine ya kufanya.Baraza
Kuu la CUF lilitangaza kumtimua Profesa Lipumba uanachama wa chama
hicho kwa madai ya kukiuka katiba, kikao hicho kilifanyika Zanzibar hivi karibuni. Kinyume Chake, Profesa Lipumba akajibu akisema hatambui kikao kilichomfukuza Zanzibar na kwamba hakikuwa halali na hakina mamlaka ya kufanya hivyo.Akadai zaidi Mkutano Mkuu wa CUF pekee ndiyo wenye Mamlaka ya kumfukuza uanachama! Alisema atakutana na Maalim Seif ofisini kwake, na yeye atakuwa amejaa amejaa tele kwenye kiti chake cha Uwenyekiti na kwamba akifika (Seif) amuone ili ampangie kazi nyingine ya kufanya. Kwa hisani ya Nipashe |
September 29, 2016
MAALIM SEIF NJOO DAR NIKUPE KAZI YA KUFANYA-PROFESA LIPUMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment