Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Balozi wa Spain
nchini Bw. Felix Costales Artieda kuhusu kusaidia kuendeleza sekta ya
Utamaduni na Michezo leo Septemba 30,2016 wakati Balozi huyo alipofika
ofisini kwa Waziri Jijini Dar es Salaam kukabidhi moja ya mradi wa
Utamaduni uliokuwa ukifanywa na serikali ya Spain katika Bonde la Ufa la
Olduvai Gorge Mkoani Manyara.
Balozi wa Spain nchini Bw. Felix
Costales Artieda (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kuhusu kuendeleza mradi wa
kujenga Shule ya Mpira wa Miguu Kigamboni kama ilivyokuwa katika mkakati
wa awali alipofika Ofisini kwa waziri Jijini Dar es Salaam Septemba
30, 2016 kumkaribisha kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Utamaduni
yaliyoandaliwa na nchi ya Spain yatakayofanyika Makumbusho ya Taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akisoma mradi wa Utamaduni
uliokuwa ukifanyika Olduvai Goerge mkoani Manyara baada ya kukabidhiwa
na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) Ofisini
kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
No comments:
Post a Comment