Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kulia, akiwahutubia wahitimu
na jumuiya ya Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)
(Hawako Pichani), wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika
katika Kituo cha Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kulia kwake
ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Bw. Pius Maneno na Mwenyekiti wa Kamati
ya Elimu na Mafunzo wa Bodi hiyo, Bi. Anne Mbughuni.
Baadhi
ya wahitimu wa taaluma ya juu ya uhasibu (CPA), wakiwa tayari
kutunukiwa shahada zao na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango,
katika Mahafali ya 38 yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichopo Bunju, nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akimkabidhi cheti cha kufanya
vizuri katika masomo ya taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T), Bi. Happiness
Ngowi, wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo yaliyofanyika Katika kituo
cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), kilichopo
Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akitangaza kuwatunuku vyeti
wahitimu wa taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T) waliofanya vizuri katika
masomo yao, wakati wa mahafali ya 38 ya NBAA, yaliyofanyika Katika kituo
cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, kilichopo Bunju,
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment