Wakati
sakata la nani ni nani ndani ya chama cha CUF Likiendelea
kuchukua sura mpya kila kukicha hatimaye leo sakata hilo limetua Mahakama Kuu ya Tanzania likiwa na sura ya kupinga kile ambacho
kinadaiwa kufanywa naMwenyekiti wa wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba.
Katika Makahakama Kuu Jijini Dar es salaam mtandao huu umeshuhudia Wakili wa
chama hicho Juma Nassor akiwa mahakamani hapo kuiwakilisha Bodi ya Wadhamini wa chama hicho ambao ndio wanafungua kesi hiyo, wakitaka Mahakama hiyo kuweka ziuo maalum kwa Msajili wa Vyama Vyavya Siasa
kuacha kufanya kazi nje ya mipaka yake ambapo pia wanamlalamikia Msajili
kuingilia maswala ya chama hicho kinyume na utaratibu.
Akizungumza
na Wanahabari nje ya Mahakama Kuu Juma Nassor amesema kuwa mbali na
kuweka zuio kwa Msajili pia kesi hiyo imewalenga
waliokuwa wanachama 12 wa CUF wakiongozwa na Profesa
Lipumba.
Hadi mtandao huu unaleta taarifa hii taratibu za kufungua keshi hiyo zilikuwa zinaendelea HABARI NA PICHA KWA HISANI YA HABARI 24 BLOG
No comments:
Post a Comment