Imefahamika kuwa hewa ya ukaa ina asilimia kubwa katika gesijoto hivyo kusababisha kumong’onyoka kwa ozoni na kupelekea kuongezeka kwa kiasi cha nyuzi joto duniani na udororaji wa uchumi wa nchi
Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa kampani ya upandaji miti ijulikanayo kama Mti Wangu katika mkao wa Dar e Salaam.
Mhe. Suluhu alisema kwa kutambua athari za ongezeko la gesi joto hususani hewa ya ukaa serikali kupitia mkoa wa Dar es Salaam imekuja na kampeni ya kupanda miti ili kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam unazalisha tani 4500 kwa kila siku zitokanazo na gesi za viwandani, vyombo vya usafiri, taka ngumu za viwandani na majumbani ikiwa ni pamoja na uchomaji na utupaji taka hovyo hivyo kupelekea serikali kwa kushirikiana na wadau kuanzisha kampeni hiyo jijini Daar es Salaam.
Alizitaja sababu nyingine za kampeni hiyo kuanzia Dar esSalaam ni pamoja na makadirio ya ongezeko la wakazi kufikia 5,895,791 kwa mwaka 2017 hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa hewa ya ukaa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji mbalimbali ya shughuli za binadamu na viwanda kwa ujumla.
Alisema tafiti mbalimbali zimeonyesha hewa ya ukaa inaongezeka jijini Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kubwa ya wakazi ambapo kwa mwaka 2015 utafiti umeonyesha mkoa huo una viwanda 1854 kati ya hivyo 480 ni vikubwa na 1374 ni vidogo.
“Nawaagiza viongozi wa Serikali, taasisi binafsi, Asasi za kiraia na kila mtanzania kwa ujumla kutunza mazingira na kupanda miti ni hatua moja mbele katika kutunza mazingira yetu,” alisema Mh. Suluhu.
Akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo, mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda alisema serikali imeweka chuma na minyororo ili kulinda wananchi kuvuka eneo ambalo si sahihi na kuweza kuhatarisha maisha yao kwa kugongwa na magari.
dsc_0220
Alisema wananchi wanapaswa kulinda vyuma hivyo kwa kuwa vinasaidia kufanya mazingira yawe mazuri na kukinga miti na nyasi zilizopandwa kando ya barabara hizo zisiharibiwe.
“Wale wanaopita usiku na wale wanaoharibu, mtu yeyote akikamatwa ameiba chuma kimoja faini yake ni kununua vyuma kumi na kuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”.