Ikiwa
imepita siku moja tangu vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) kutangaza kutomtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti
halali wa Chama cha Wananchi (CUF).
Mapema
asubuhi jana wakati kikao cha Ukawa kinaendelea, Lipumba alitengua
uteuzi wa baadhi ya wakurugenzi na manaibu wakurugenzi aliodai kuwa
aliwateua kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Na kudai kwamba, kwa kuwa yeye ni mwenyekiti ana mamlaka ya kutengua teuzi alizofanya.
Wakurugenzi
aliodai kutengua teuzi zake ni Ismail Jusa Raju ambaye ni Mkurugenzi wa
Mambo ya Nje pamoja na Naibu wake Abdallah Mtolea. Mwengine ni
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shaweji Mketo.
Wengine
ni Kuruthumu Mchuchuri ambaye ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na
Sheria pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mustafa Wandwi.
Hata
hivyo, Modewjiblog.com iliwatafuta baadhi ya wakurugenzi waliodaiwa
kuvuliwa wadhifa na Lipumba na kubahatika kuzungumza na Kuruthumu
Mchuchuri. Mchuchuri ameuambia mtandao wa huu kuwa Lipumba hana mamlaka
ya kutengua ukurugenzi wake.
Ameeleza
kwamba, katiba ya CUF inasema kuwa, ili mkurugenzi mpya aidhinishwe na
au aliyekuwepo atenguliwe wadhifa wake, inabidi Baraza Kuu la Uongozi
Taifa la CUF lithibitishe uteuzi mpya au utenguzi wa mkurugenzi aliyepo.
Amesema,
Lipumba hatofanikiwa kuteua wakurugenzi wapya kutokana kwamba hana
baraza halali litakalothibitisha uteuzi wa atakaye mteua na utenguzi
wake.
“Lipumba
hana baraza kuu la kunitengua na au kuthibitisha mkurugenzi yeyote
atakayemteua. Kwanza wajumbe halali wa baraza hilo zaidi ya 40 wamepiga
kura ya kumtoa katika chama,” amesema Mchuchuri.
Ameongeza
kuwa “Lipumba amestaafu na analitambua hilo na ndiyo maana awali kila
akiandika barua ya kuhitaji lolote kutoka katika chama anajitambulisha
kama mwenyekiti mstaafu. Kwa ufupi siasa kwa upande wake imemkalia
vibaya hana jinsi,” amesema.
Modewjiblog.com haikuishia hapo, ilimtafuta Mketo kwa njia ya simu kwa ajili ya mahojiano zaidi lakini hakupatikana MO BLOG
No comments:
Post a Comment