DR Congo imeitwanga
Morocco 1-0 na kuandika ushindi waPili katika michuano ya Afcon 2017
inayofanyika nchini Gabon baada ya Senegal kuwa timu ya kwanza kushinda.
DR.Congo walipata ushindi huo kupitia bao la Junior Kabananga aliyefunga katika dakika ya 55.
Hata hivyo, Morocco ndiyo waliokuwa wakishambulia zaidi kuliko DR Congo waliokuwa makini katika kujilinda.
DR Congo walipata
pengo baada ya Lomalisa Mutambala aliyeingia katika dakika ya 64
kulambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu katika dakika ya 85.
Kipa Matambi ambaye ni kipa wa TP Mazembe, alikuwa kikwazo kikubwa kwa Morocco ambao walishambulia zaidi.
Kwa ushindi huo,
DR Congo sasa wanaongoza kundi C wakiwa na pointi tatu na kufuatiwa na
Ivory Coast, Togo ambao kila mmoja ana pointi moja huku Morocco akiwa
anaburuza mkia akiwa hana kitu.
No comments:
Post a Comment