Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amewasimamisha kazi watendaji watatu
wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani hapa, ili kupisha uchunguzi wa
matumizi ya fedha zaidi ya sh. milioni 300, zilizotolewa na Benki ya
Dunia kwa ajili ya maendeleo wilayani humo.
Waliosimamishwa
kazi ni pamoja na mweka hazina, mchumi na Mhandisi wa Halmashauri hiyo.
Kwa pamoja wanadaiwa kubadili matumizi ya fedha za kutekeleza miradi ya
SEDEP, zilizotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kuboresha mazingira ya
kusomea wanafunzi wa shule za sekondari.
Akizungumza
akiwa katika ziara wilayani humo juzi, Mongela alisema ni lazima
uchunguzi wa kina ufanyike, kwani thamani ya vyumba vya madarasa na vyoo
vilivyojengwa kutokana na fedha za mradi huo, hailingani na fedha
zilizotumika.
“Kunzia
Jumatatu (leo), kuna timu ya wakaguzi itakuja hapa Magu kukagua na
kuchunguza thamani ya fedha zilizotumika kwenye miradi hii ambayo
nimeikagua. Miradi hii inajumuisha miradi ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa na vyoo ambayo inaonyesha wazi kuna uchakachuaji umefanyika,”alisema Mongela.
Mkuu
Wilaya ya Magu, Hadija Nyembo alisema mambo yaliyokwamisha miradi ya
ujenzi huo ni kuelekeza fedha hizo katika ujenzi wa maabara tofauti na
matumizi ya fedha yalivyopangwa.
Hata
hivyo, mabadiliko ya matumizi ya fedha hizo, yanadaiwa kuwa yalifanyika
bila kuthibitishwa na Wizara ya Fedha na Mipango ili yapewe baraka kwa
kuwa Wizara hiyo, ndio yenye mamlaka ya kutoa idhini ya mwisho ya
matumizi ya fedha za Umma.
Kutokana
na sababu hizo mkuu huyo wa Mkoa aligoma kuzindua vyumba viwili vya
madarasa vya shule ya msingi Nyanguge vilivyojengwa kupitia kiasi hicho
cha fedha, kutokana na madai kuwa vyumba hivyo pamoja na ujenzi wa vyoo
vimejengwa chini ya kiwango.
No comments:
Post a Comment