Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umewataka watanzania
kuwapuuza Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye na Waziri Mkuu
aliyejiuzulu Edward lowassa kuwa wanaota ndoto za mchana .
Umoja
huo umesema kuwa kuiombea CCM kushindwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ni
sawa na kujivisha akili za Abunuasi,ambaye mipango haitimii, aidha umoja
huo umesema upinzani wa Tanzania haukubaliki mbele ya wananchi
wazalendo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa
akihutubia katika mkutano wa kampeni katika kata ya kiwanja cha ndege
mkoani Morogoro.
Alisema
kuwa wananchi hawana budi kuwapuuza Lowassa, Sumaye na chama chao kwa
sababu sio viongozi waadilifu bali ni wasaka madaraka.
“Watanzania
wapuuzeni watu hawa kwa sababu Sumaye ni Pwagu na mwenzake Lowassa ni
pwaguzi, wanahaha usiku na mchana kusaka madaraka wakati wananchi
wanawajua sio waadilifu na hawaaminiki katika jamii,”alisema Shaka.
No comments:
Post a Comment