·
Ni gawio la faida ya kutumia M-Pesa kwa watumiaji zaidi ya Milioni 7
Dar es Salaam, Monday January 16, 2017:
Wakati
wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya
Nogesha Upendo ya Vodacom katika kujishindia mamilioni ya fedha kila
siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye
simu zao, sasa malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo yameanza wiki
hii yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya
wateja na mawakala wa M-Pesa.
Awamu
hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh
Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri
ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya
akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na
yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya
Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida
ya gawio hilo kampuni hiyo imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39
katika awamu zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii
itakapokamilika, Ni zaidi ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa
moja kwenye mifuko ya wateja wetu.
‘Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”.
Kila
mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo
atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua
vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake.
Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio
kubwa Zaidi la faida’ Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi mtendaji wa
Vodacom Tanzania.
Kuona
kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea
SMS inayoonyesha kiasi chako. Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu
vinaweza kununuliwa kwa kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi
kwa kutumia pesa uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA
MAONGEZI/VIFURUSHI kisha chagua kifurushi unachohitaji.
Promosheni ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya
7 sasa ambapo Zaidi ya wateja
200 washajishinidia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na
600 wengine wameshashinda Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea
kuongeza nafasi za kushinda zawadi za siku na wiki za hadi Tsh Milioni
1/- mteja anatakiwa kununua kifurushi chochote cha Vodacom ambapo
ataingia kwenye droo moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment