Mwili wa mwandishi wa habari za
michezo wa gazeti la uhuru na mzalendo Amina Athuman ukisafirishwa
asubuhi hii na boti ya Kilimanjaro kuelekea Dar es Salaam na
utasafirishwa tena kijijini kwao Lushoto kwa mazishi yanayotarajiwa
kufanyika siku ya jumanne mchana.
Marehemu alikuwa Zanzibar kikazi
akiripori habari za michezo Kombe la Mapinduzi aliugua uchungu na baada
ya kujifungua mtoto wa kiume kwa bahati mbaya mtoto amefariki baada ya
kuzaliwa na yeye akapata kifafa cha uzazi na kufariki jana asubuhi.
Mwenyenzi mungu ampe kauli thabiti na amsamehe madhambi yake Ameen
|
January 16, 2017
MWILI WA MWANAHABARI MAREHEMU AMINA ATHUMAN WASAFIRISHWA LEO KUJA DAR ES SALAAM NA KISHA MKOANI TANGA KWA MAZISHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment