Jarida
la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi
wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo
ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao
walikuwa wakiwania.
Baada
ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka
mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8.
MO
Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa
Ghana, John Mahama ambaye amepata apata asilimia 38.3.
Kwasasa
bado Jarida la African Leadership bado hawajatoa taarifa ni lini
watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine
Person Of The Year 2016.
|
January 16, 2017
ZOEZI LA KUCHAGUA MSHINDI WA TUZO YA ALM 2016 LAFUNGWA,MO DEWJI AONGOZA KWA ASILIMIA 60.8
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment