Baada
ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa Serikali za
mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri kwa
wenyekiti wa serikali za mitaa.
Akizungumza
leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali za mitaa,
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene amesema
amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa Wenyeviti
wa serikali za mitaa mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.
''Hakukuwa
na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti,
lakini kama mihuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona kufuta
muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili" amesema
Sanjari
na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu za
msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na matumizi
mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea kuigawa
ardhi bila utaratibu maalumu.
No comments:
Post a Comment