Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo
mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana
na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na
uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na
kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya linaongeza jitihada kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama
katika kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva
na watumiaji wengine wa barabara wanatii, wanaheshimu na kufuata sheria
za usalama barabarani. Aidha kumekuwa na tukio 01 la ajali ya vifo kama
ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 18.01.2017 majira ya
saa 20:30 usiku huko Kijiji cha Kongolo – Mswiswi, Kata ya Chimala,
Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Gari yenye namba za
usajili T.348 DEK aina ya Mitsubishi Fuso likiendeshwa na Dereva aitwaye
DEO MGAYA [25] Mkazi wa Mbeya liligongana na Gari lenye namba za
usajili T.321 DAK aina ya Nissan Diesel Basi Mali ya Kampuni ya Taqwa
lililokuwa likiendeshwa na Dereva aitwaye HAMIS HASSAN [62] Mkazi wa Dar
es Salaam lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Lubumbashi Nchini
Kongo na kupoteza uelekeo na kugonga Gari nyingine yenye namba za
usajili T.143 BUK lenye Tela T.911 BXN aina ya Leyland DAF lililokuwa
likiendeshwa na Dereva aitwaye BURHANI SULEIMAN [42] Mkazi wa Chimala na
kusababisha vifo vya watu watatu.
Watu waliofariki katika ajali hiyo
ni 1. HAMZA IBRAHIM ambaye alikuwa Dereva Msaidizi wa Gari lenye namba
za usajili T.321 DAK aina ya Nissan Diesel Basi 2. SHIZYA HONJAS [24]
ambaye alikuwa Dereva Msaidizi wa Gari lenye namba za usajili T.348 DEK
aina ya Mitsubishi Fuso na 3. Mwanamke mmoja ambaye bado hajatambuliwa.
Aidha katika ajali hiyo watu 16
walipata majeraha, majeruhi 08 walitibiwa na kuruhusiwa na majeruhi 08
wamelazwa katika Hospitali ya Mission Chimala kati yao 07 ni wanaume na
01 ni mwanamke ambao ni 1. HUSSEIN MWANJALI [51] Mkazi wa DSM 2. ADEN
JASON MWAMBANDE [32] Mkazi wa Kyela 3. SHABANI ALLY [30] Mkazi wa DSM 4.
KAPINGA DOMINICK [32] Mkazi wa Afrika Kusini.
Majeruhi wengine waliolazwa ni 5.
SHABANI MOHAMED [36] Mkazi wa DSM 6. LUGANO HAKSON [27] Mkazi wa Mbalizi
Mbeya 7. LUYAMBA MHUMBI MALYETI [45] Mkazi wa Lubumbashi – Kongo na 8.
KALENGA KABANGE [39] Mkazi wa Kongo.
Miili ya marehemu imehifadhiwa
katika Hospitali ya Rufaa Mbeya. Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva
Gari yenye namba za usajili T.348 DEK aina ya Mitsubishi Fuso kutaka
kulipita Gari la mbele yake bila kuchukua tahadhari na mwendo kasi wa
Dereva wa Basi.
WITO:
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa
madereva kuwa makini ikiwa ni pamoja na kufuata sheria, alama na michoro
ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.
Imesainiwa na:
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
January 19, 2017
TAARIFA TOKA JESHI LA POLISI MKOANI WA MBEYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment