Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Nishati na Madini, Doto Mashaka Biteko (wa pili kushoto) akimsikiliza
Meneja wa Mgodi wa Buzwagi, Assa Mwaipopo (hayupo pichani) akielezea
shughuli za uzalishaji wa Dhahabu katika Mgodi huo. Kushoto kwake ni
Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na wengine ni wajumbe wa
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Watumishi kutoka Wizara
ya Nishati na Madini na Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi.
Kaimu Kamishna wa Nishati na
Madini, Ally Samaje (anayetoa maelezo) akielezea Mpango wa Serekali
wakati wa kufunga Mgodi wa Buzwagi. Wengine katika picha ni Wabunge
kutoka Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Watumishi wa Wizara ya
Nishati na Madini na Viongozi Waandamizi kutoka Mgodi wa Buzwagi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Profesa James Ntalikwa (katikati) akiwa anafanya majadiliano
na Kaimu Kamishna wa Madini, Ally Samaje na Mbuge wa Kahama Jumanne
Kishimba Mara baada ya kutembelea mgodi wa Buzwagi.
Wataalamu kutoka Idara ya Madini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka katika eneo la uzalishaji wa Dhahabu.
Muonekano wa Mgodi wa Buzwagi katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,
Kotena iliyofanyiwa maandalizi tayari kupokea makinikia ya Shaba ambayo yanachimbwa kwa asilimia kubwa katika Mgodi wa Buzwagi.
Kotena ambayo tayari imejazwa na makinikia ya Shaba tayari kwa ajili ya kufunga ili kusafirishwa nje.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Profesa James Ntalikwa (wa pili kushoto) akimsikiliza Kaimu
Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, kabla ya kusikiliza mada kutoka
kwa Meneja wa Buzwagi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Nishati na Madini, Doto Mashaka Biteko (wa pili kulia) akiwa na
wanakamati wezake wakiongozana na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya
Nishati na Madini na Mgodi wa Buzwagi mara tu baada ya kuwasili katika
Mgodi huo.
……………………
|
January 19, 2017
MGODI WA BUZWAGI MBIONI KUFUNGWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment