Leo
mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezungumza akiwa kituo cha
kati cha Polisi Dar es salaam pembeni ya Kamishna Simon Sirro kuhusu
ishu ya dawa za kulevya inayoendelea kwenye headlines.
Mambo
aliyoyasema mkuu wa mkoa Paul Makonda leo ni kutoa siku kumi kuanzia
kesho February 7 2017 kwa Wenyeviti wa mtaa, Wazazi na Watumiaji na
Wafanyabiashara.
==>Natoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya.
==>Natoa
siku 10 kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto
anatumia dawa za kulevya na unaishi nae, njoo utoe taarifa…..
tukikukamata baada ya siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe
ulikua sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya.
==>Natoa
siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje
wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekua ukifanya biashara ya dawa za
kulevya na umeacha njoo Polisi, nguvu tunayo, uwezo tunao…. hakuna
kiunga tutashindwa kufika, hizi kelele nyingine zinatupa hamasa
|
February 6, 2017
ALICHOKISEMA LEO RC PAUL MAKONDA AKIWA POLISI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment