KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 7, 2017

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE BUNGENI KUHUSU SAKATA LA WEMA SEPETU KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) amesema Serikali imeshindwa vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa kutokiwezesha chombo kilichoundwa na sheria ili kupambana nayo.

“Kamati (ya Bunge) imelalamika kuwa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ina bajeti finyu na hata hiyo bajeti haitolewi na hivyo kusababisha Mamlaka kukosa vitendea kazi, kushindwa kutoa elimu kwa umma, kushindwa kufanya operesheni za ukamataji wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na kushindwa kutoa ushauri nasaha kwa waathirika,” alisema Zitto.

Zitto alikuwa akizungumzia taarifa ya Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi imebaini dosari nyingi katika sera ya dawa za kulevya ya mwaka 2004 ambayo imepitwa na wakati.

Wakichangia katika taarifa ya shughuli za kamati kwa mwaka 2016/17, wabunge, akiwemo Zitto, walisema dawa za kulevya ni janga la taifa na linahitaji mikakati ya kupambana na siyo kuwaweka rumande waathirika ambao wanahitaji kupatiwa matibabu.

Zitto alibainisha kuwa watuhumiwa waliokamatwa katika vita inayoendelea jijini Dar es Salaam  wamelazwa ndani kwa zaidi ya siku tatu bila kufikishwa mahakamani.

“Baadhi ya watuhumiwa wameelezwa kuteswa na kupigwa na polisi na kulazimishwa kutoa maelezo kwa Polisi," alisema Zitto. "Umma haujaelezwa kama watu hawa wamekamatwa na madawa hayo ama wamehisiwa kuwa ni watumiaji tu.”

No comments:

Post a Comment