Katibu wa UWT wilaya ya Bagamoyo,Mwatabu Hussein (kulia)aliyemshika mgombea wa uenyekiti kitongoji cha Magomeni B Rajabu Swedy,wakishangilia baada ya kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa kitongoji hicho. |
Mwenyekiti wa UWT Bagamoyo,Apsa Kilingo akizungumza jambo wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo kitongoji cha Magomeni B,kata ya Nianjema. |
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya CCM ,wilayani Bagamoyo,Abdul Sharif ,ambae pia ni meneja kampeni wa uchaguzi mdogo kitongoji cha Magomeni B,kata ya Nianjema,akizungumza jambo kwenye uzinduzi wa kampeni hizo.(picha na Mwamvua Mwinyi) |
Mwenyekiti wa CCM
Bagamoyo,Almas Maskuz wa kulia akimnadi ,mgombea wa nafasi ya mwenyekiti
wa kitongoji cha Magomeni B kata ya Nianjema wa kushoto Rajabu Swedy
.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WANANCHI na wanaCCM wilayani
Bagamoyo,wametakiwa wasijaribu wala kufanya makosa kuchagua vyama vya
upinzani katika uchaguzi mdogo wa vitongoji ikiwemo cha Magomeni B .
Kimesema hakikubahatisha
kumsimamisha Rajab Swedy(M-baga)kuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa
kitongoji hicho kwani kinaamini ana uwezo na sifa za kiuongozi.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya
chama cha mapinduzi wilaya ya Bagamoyo,Abdul Sharif aliyasema hayo
wakati akimnadi mgombea huyo kwa wananchi.
Alieleza kwamba,Swedy ni kijana makini,msomi na mpenda maendeleo hivyo ana uwezo wa kukiongoza kitongoji hi
Aidha Sharif alisema CCM
imesimamia ilani yake kikamilifu na kuitendea haki katika kutatua kero
za wananchi ndani ya miaka 40 iliyopita.
Hata hivyo alisema, CCM bado ina
nguvu ya kuongoza kuanzia ngazi za chini kwani kinatekeleza ilani yake
na kushughulikia kero za wananchi na kujali watu wanyonge.
“Vyama vya upinzani vinaonyesha udhaifu tangu chini kutokana kushindwa kuwatumikia wananchi ”alisema .
Sharif ambae pia ni meneja wa
kampeni ya mgombea wa kitongoji cha Magomeni B,alisema vyama vya
upinzani havina nafasi kwa sasa kwani CCM inaonekana inavyofanyakazi
kupitia viongozi wake wanaowajibika ipasavyo.
Nae mwenyekiti wa CCM
Bagamoyo,Almas Maskuzi aliwaomba wananchi wa kitongoji cha Magomeni
B,kumchagua Rajab Swedy kuwa mwenyekiti wao wa kitongoji .
Alisema CCM wilaya,imejipanga
kushinda katika chaguzi zote ndogo za nafasi ya vitongoji vitatu
vinavyorudia uchaguzi ikiwemo Mwavi ,Zinga na Magomeni B.
Maskuzi alisema ni wakati wa
wanaCCM kusaka kura nyingi kwa wananchi kwa kuwanadi wagombea
waliosimamishwa na kueleza sifa za chama cha mapinduzi na yale ambayo
imekwisha yafanya.
Kwa upande wake mgombea wa
kitongoji hicho,Rajabu Swedy aliahidi kutatua ama kusimamia kero ya maji
na barabara ambazo zinasumbua kwenye eneo hilo kipindi kirefu sasa.
Swedy aliomba kura kwa wapenzi wa
CCM,wananchi na wanaCCM wote bila kujali itikadi za kisiasa na kusema
ataomba ushirikiano wao endapo watamchagua.
Uchaguzi huo,unatarajiwa kufanyika
februari 19 mwaka huu katika vitongoji vyote ambavyo vinapaswa kurejea
uchaguzi huo kwa mujibu wa taratibu na sheria.
|
No comments:
Post a Comment