Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akiwasilisha hoja katika mkutano wa Tano wa Bunge linaloendelea Mjini
Dodoma.
……………………………………………………………
Na mwandishi wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia vijana kutambua na
kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo nchini ili
kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na kutimiza adhma ya kuleta
maendeleo hususani kwa vijana.
Mhe. Mhagama ameyasema
hayo jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni Mhe. Maulid
Mtulia iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua tatizo la
ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge
unaoendelea Mkoani Dodoma.
Katika Mkutano huo Mhe. Waziri
alisisitiza kuwa Serikali ina mipango na mikakati madhubuti
inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania ili kujiletea maendeleo
yao wenyewe na kuondokana na umasikini.
“Serikali ya Awamu ya Tano
imeendelea kuweka mikakati ikiwemo uwanzishwaji wa programu mbalimbali
zitakazo saidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuangalia
matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zimepelekea kuwa na programu
zinazolenga kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana” Alisema
Waziri
Alisisitiza kuwa programu hizo ni
pamoja na; kurasmisha ujuzi usio rasmi kuwa rasmi, mfumo wa mafunzo kwa
vitendo, mfumo wa uanangezi pamoja na kukuza mafunzo kwa watanzania
kulingana na soko lililopo kwa sasa.
Pamoja na juhudi hizo
zinazotarajiwa kuzaa matunda bado Waziri aliwatoa hofu wananchi wote kwa
kuwepo kwa fursa hizo za ajira zitakazo jali hali za watu pasipo
kuangalia makabila yao, rangi wala dini.
“Katika kutatua changamoto ya
ajira kwa vijana hatuta angalia kabila, rangi wala dini ya mtu bali
kutakuwa na haki na usawa”.Alisisitiza Waziri
Aliongezea kuwa, Serikali pia
inajitihada za kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na urasimishaji
wa sekta isiyo rasmi ili kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.
“Serikali itatumia sekta zenye
uwezo wa kutoa ajira kwa wingi ikiwemo zile za Kilimo, majenzi,
Mawasiliano na Utalii ili kuzitumia kuweka mazingira mazuri kwa vijana
kupata fursa za ajira”.
Mhe. Mhagama alisisitizia bungeni
kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika zitatumika kama chachu
ya kuangalia maeneo yanayohitaji kusaidia kwa haraka na kupunguza
changamoto hiyo kwa vijana.
“Kwa kuangalia tafiti ya Hali ya
Ajira Nchini ya mwaka 2014 imeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira
kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014
na ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka
2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014”,alisema.
Hata hivyo, Waziri Mhagama
alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo Serikali bado ina wajibu wa
kuongeza jitihada zaidi ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa ajira na
kuboresha maisha ya vijana.
|
February 6, 2017
SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA AJIRA KWA VIJANA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment