Kocha wa zamani wa
Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema yupo tayari kurejea kujihusisha
na soka kwa mara nyingine baada ya kustaafu kwa muda kwa kuomba
akabidhiwe majukumu ya ukatibu mkuu wa Simba.
Awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Patrick Kahemele ambaye aliamua kujiuzulu na kurejea Azam TV wiki iliyopita.
Julio aliyewahi kuwa
kocha msaidizi wa Simba kwa nyakati tofauti alijiweka pembeni
kujihusisha na masuala ya soka na kuikacha timu yake ya Mwadui baada ya
kuchoshwa na maamuzi mabovu ya waamuzi wa ligi kuu.
Julio amesema kuwa
kwa upande wake hana wasiwasi endapo viongozi wa Simba wakiongozwa na
rais wake, Evans Aveva wakiamua kumpa nafasi hiyo kwani anaamini ana
uwezo wa kuongoza.
“Siyo kama najipigia
chapuo lakini kama viongozi wa Simba wakiamua kunipa nafasi ya ukatibu
sitaweza kukataa kwa sababu naipenda timu hiyo na kila mmoja anajua na
kama nikiwepo naamini nitaongezea kitu fulani na kuifanya timu ipate
matokeo mazuri.
“Uzuri wangu kwangu
kwamba sikufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na soka hivyo hata
nikirejea hakuna ambaye atashtuka na niwaahidi kwamba nitaitumikia
nafasi hiyo kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa kipindi kirefu,”
alisema Julio.
SOURCE: CHAMPIONI
|
February 8, 2017
JULIO KUCHUKUA NAFASI YA KAHEMELE,SASA KUWA KATIBU MKUU SIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment