Mwenyekiti wa Yanga,
Yusuf Manji kesho amepanga kwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha
jijini Dar es Salaam maarufu kama “Centre” kesho badala ya keshokutwa .
Manji ameyasema hayo
hivi punde saa chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Polisi wa Dar es Salaam ,
Paul Makonda kutangaza majina 65 ya wanaotakiwa kufika kwenye kituo cha
hicho kikubwa cha Polisi ili kusaidia vita ya kupambana na madawa ya
kulevya kama sehemu ya wanaotumihumiwa au la.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Manji alisema kuwa hawezi
kubadili ratiba zake keshokutwa na kwenda kupanga foleni ya watu 65 kwa
ajili ya kitu hicho.
Manji alisema, ana
kazi nyingi za kufanya hiyo keshokutwa ijumaa, hivyo ataenda kesho
asubuhi na mapema sana ili kutekeleza suala hilo aliloitiwa.
Pamoja na kukubali
kwenda tena mapema, Manji amesema amepanga kuchukua hatua za kisheria
kwa kwenda mahamakani kwa ajili ya kumfungulia mashtaka Makonda.
“Mimi nitaenda kituo cha Polisi kesho asubuhi na mapema na sisubiri hiyo Ijumaa anayotaka yeye Makonda naomba nieleweke.
“Baada ya kutoa huo
ushirikiano Polisi, basi nitaenda mahakamani kumfungulia mashtaka
Makonda kwa kunidhalilisha kwa kutumia vibaya jina langu, kwani kitendo
cha kutumia jina la mtu vibaya ni makosa na katiba ya nchi inaniruhusu
kumshtaki Makonda,” alisema Manji.
“Kama kweli mtu
unamuita kukusaidia kwa ajili ya madawa ya kulevya, vipi unamtangaza
mbele ya hadhara. Akishakutajia utaweza vipi kumlinda muda wote,
ingekuwa vizuri kumuita kimyakimya, halafu akutajie na wewe ufanyie kazi
hasa kama uliona anajua,” alisema.
“Kweli nitakwenda Alhamisi, niko tayari kupimwa na kusachiwa. Lakini ningependa na Makonda apimwe pia na kusachiwa.
“Sikatai kuwepo na
vita ya madawa, lakini hauwezi ukafanya kila kitu bila ya kujali haki za
watu, heshima zao, majina yao. Hii si sawa na siwezi kukubali.”
No comments:
Post a Comment