Vodacom
Tanzania tunapenda kuwajulisha wateja wetu na wananchi wote kwa ujumla
kuwa bado tunaendelea na zoezi letu la kuwapatia wateja wetu malipo
ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo tulianza mwezi Januari nakufanya
yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja
wetu na mawakala wa M-Pesa kwa ujumla.
Akiongea
na mtandao huu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom
Tanzania, Jacquiline Materu alisema Mpaka sasa tumeweza kuwagawia
wateja wetu kiasi cha shilingi Bilioni 6/- ikiwa hii ni awamu ya kwanza
ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa kutakuwa na awamu tatu za
ugawaji wa fedha hizo ambapo awamu ya kwanza tayari imefanyika na awamu
zingine zitaendelea mpaka mwezi wa tatu na kukamilisha
zoezi zima la ugawaji wa billionii 32 kwa wateja wetu,Alisema Materu
“Napenda
kuwahakikishia wateja wetu wote kwa ujumla ya kana kwamba Malipo haya
yanafanyika kwa awamu kwa hiyo wasiwe na wasiwasi kwani yatawanufaisha
wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania,Ugawaji huu
wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa
dhana kuu ya mtandao wetu tuliojiwekea”,Alisema Materu.
No comments:
Post a Comment