Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mery Majaliwa wakikabidhi zawadi ya chakula kwa wazee na walemavu waishio kambi ya Sukamahela iliyopo wilayani Manyoni, wa kwaza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi. |
Mmoja wa wazee waishio kambi ya Sukamahela akizungumza na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mery Majaliwa baada ya kukabidhi zawadi ya chakula kwa wazee na walemavu waishio kambi ya hiyo iliyopo wilayani Manyoni. |
Baadhi ya chakula kilichotolewa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mery Majaliwa kwa wazee na walemavu waishio kambi ya Sukamahela iliyopo wilayani Manyoni, chakula chote kilichotolewa ni tani 7.5 za mahindi, maharage na mchele. |
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mery
Majaliwa wakitembelea makazi ya wazee na walemavu waishio kambi ya
Sukamahela iliyopo wilayani Manyoni.
……………
Wazee na walemavu waishio kwenye
kambi ya Wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni, Mkoani Singida,
jana 13 Februari 2017, wametembelewa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na kupokea msaada wa tani 7.5 za vyakula
ambavyo ni mchele, unga wa sembe na maharage.
Akikabidhi
msaada huo kituoni hapo Mama Janeth amemtaka msimamizi wa kituo hicho
Bw. Jeremia Mgoo kuhakikisha chakula hicho kinatumika kwa matumizi
yaliyokusudiwa na hakichakachuliwi.
“Viongozi
naomba mfuatilie chakula hiki na kuhakikisha kinatunzwa na kutumika
vizuri, ili kiwafae Wazee wetu hawa ambao jamii imewasahau, na mimi
binafsi jicho langu litakuwa hapa kufuatilia ili kuhakikisha
hakichakachuliwi na atakaefanya kinyume tutamshughulikia” amesema Mama
Janeth.
Mke
wa Rais pia amewaomba wadau mbali mbali nchini na watu wote wenye
mapenzi mema kujitolea kuwasaidia Wazee na watu wasiojiweza waishio
katika makambi ya kulelea Wazee kote nchini kwani Wazee hawa ni kundi
lililosahaulika na wamekuwa na changamoto zinazofanana ilihali hakuna
anaekumbuka kujitolea kuwasaidia hivyo kuishi katika mazingira magumu.
Nae
Mama Mary Majaliwa akizungumza kambini hapo amesisitiza wadau
mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee waishio katika makambi ya
kulelea walemavu na wasiojiweza kote nchini.
“Watanzania wajenge tabia ya
kuwakumbuka na kuendelea kuwasaidia Wazee hawa kama tulivyofanya sisi
ili nao wajisikie kupendwa na wanajamii wenzao” amesema.
Wakati
huo huo msimamizi wa Makazi hayo Bw. Jeremia Mgoo amesema kituo hicho
kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la
kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida huku
akibainisha changamoto zinazokikabili kituo hiko kuwa ni upungufu wa
wapishi kwani kituo kinampishi mmoja tu hali inayopelekea Wazee hao
kupikiwa mlo mmoja tu kwa siku na uchakavu wa nyumba wanazoishi Wazee
hao.
Akitoa
shukrani zake kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Wazee waishio kambini
hapo, Mzee Andrea Yohana ameshukuru kwa msaada huo wa chakula kutoka
kwa Mhe. Mama Janeth Magufuli akisindikizwa na Mama Mary Majaliwa na
kuwaomba wasichoke kuja kuwaona tena na kuwapa msaada kila
wanapojaaliwa.
|
No comments:
Post a Comment