WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka watumishi wa umma nchini wawe wabunifu katika kusaidia
kutafuta vyanzo vya mapato kwenye jamii inayowazunguka.
Ametoa wito huo leo (Jumanne,
Februari 14, 2017) ofisini kwake mjini Dodoma mara baada ya kupokea
mchango wa sh. milioni 5.6 kwa ajili ya kununulia madawati 70 kutoka kwa
watumishi wa TAMISEMI – Dodoma.
Amesema ubunifu huo uliofanywa na
watumishi wa TAMISEMI, ni mfano mzuri wa kuigwa na watumishi wengine
nchini kwani utaisaidia Serikali kuleta maendeleo.
“Hii ni mara ya tatu kwa TAMISEMI
kuchangia huduma za jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini… lakini pia
niwashukuru kwa kuchagua jimbo la Ruangwa kuwa miongoni mwa maeneo
ambayo ni wanufaika wa mchango wenu,” amesema.
“Mchango huu ni mkubwa na
utasaidia mikondo miwili kwa shule za sekondari. Tunahitaji kupata
mawazo mapya kama haya, na tunahitaji wafanyakazi wengine wajifunze
kutoka TAMISEMI,” amesema.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhi mchango wao, kiongozi wa ujumbe ulioenda kuwasilisha mchango
kwa Waziri Mkuu, Bw. Filbert Rwakilomba amesema lengo lao ni kuchangia
madawati 100 lakini wameamua kutanguliza mchango wa madawati 70 na baada
ya siku mbili watakabidhi mchango wa madawati 30 yaliyobakia.
Bw. Rwakilomba ambaye anaongoza
kamati ya watu 30 ambao ni watumishi kutoka idara tofauti za Ofisi ya
Rais TAMISEMI Dodoma, amesema wametoa mchango huo kama ishara ya kuenzi
kazi aliyoifanya Waziri Mkuu Majaliwa wakati akiwa Naibu Waziri
(TAMISEMI – Elimu).
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMANNE, FEBRUARI 14, 2017.
|
February 14, 2017
WAZIRI MKUU APOKEA SH. MILIONI 5.6 ZA MADAWATI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment