KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 15, 2017

PSG YAIPIGA 4G BARCELONA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA

PSGGG
Mabingwa wa nchini Ufaransa timu ya PSG imefanya maafa baada ya kuitwanga Barcelona kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya.
Barcelona ikiwa ugenini jijini Paris imeshindwa kuonyesha cheche licha ya kuongozwa na nyota wake Lionel Messi na Neymar na kujikuta ikipokea kipigo hicho cha kondoo mchovu.
Angelo Di Maria ametumbukia nyavuni mara mbili huku Endson Cavani aliyetimiza miaka 30 jana akifunga moja na Julian Draxler akifunga moja.
Mechi nyingine Benfica imeifunga Borussia Dortmund kwa bao 1-0.
Michuano hiyo itaendelea tena leo kwa Michezo miwili Bayern Munich watawaalika Arsenal huku Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Real Madrid watacheza na Napoli toka Italia

No comments:

Post a Comment