Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Maruwa wilaya ya Moshi vijijini mara baada ya kuwasili kwa ajili ya shughuli ya kuotesha miti 120 katika eneo la nusu maili lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. |
Kaimu Mwenyekiti wa Shirika
lisilo la Kiserikali la kuhifadhi Mazingira (TEACA) Adoncome Mcharo
akitoa taarifa fupi ya ukuaji wa miti iliyooteshwa katika eneo na nusu
maili ,Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa Mratibu wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na ujumbe wake (hawapo pichani) |
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi Celestine Mushi akionesha eneo ambalo lilipandwa miti na tayari imeanza kukua. |
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi Celestine Mushi akiotesha miche ya miti katika eneo hilo. |
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akimwagia maji miti aliyootesha katika eneo hilo. |
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Kimataifa (UN) nchini ,Hoyce Temu akiotesha mti na kumwagia maji wakati wa zoezi la kuotesha miti katika eneo la Nusu Maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. |
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiotesha mti katika eneo hilo huku balozi Mushi akishuhudia. |
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez kwa pamoja na Balozi Mushi wakimwagia maji katika mti uliooteshwa katika eneo la Nusu Maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. |
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiwa na Balozi Mushi katika alama ya kumbukumbu ya UN iliyokwa katika eneo hilo la nusu maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. |
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kulamizika kwa zoezi la uoteshaji miti ,eneo la nusu maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
|
No comments:
Post a Comment