Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga,
Yusuf Manji ni mmoja wa watu maarufu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar,
kuwa wanahitajika keshokutwa Ijumaa kwenye kituo kikuu cha polisi kwa
ajili ya mahojiano kuhusiana na madawa ya kulevya.
Makonda ametaja orodha ya majina kadhaa marufu kati ya 65
aliyodai kuwa anayo katika orodha yake ya wanaotakiwa kufika kituoni
hapo kwa ajili ya zoezi hilo la mahojiano katika kampeni yake ya
kuendeleza kupambana na utumiaji na biashara ya madawa ya kulevya.
Akizungumza na waandishi wa
habari kwenye ofisi zake leo jijini Dar, Makonda alimtaja Manji kuwa
anatakiwa kufika kituoni hapo Ijumaa hii, pia alimtaja mbunge wa zamani
wa Kinondoni, Iddi Azzan ambaye alikuwa kipa wa timu ya wabunge na timu
ya wabunge wa Simba wakati alipokuwa mbunge.
Majina mengine maarufu yaliyopo
katika orodha hiyo ni na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein
Pambakali, Mbunge wa Hai, Freeman Aikaely Mbowe, Mchungaji Josephat
Gwajima.
Ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya
wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa
muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara
hiyo.
Watu hao watahojiwa na polisi
kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza
iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.
Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.
Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.
|
February 8, 2017
SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, MAKONDA AMTAJA MANJI, AMTAKA KUFIKA POLISI KUHOJIWA SIKU YA IJUMAA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment