Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa sare za Jeshi kwa
viongozi wanajeshi wanaoteuliwa na kupewa madaraka mbalimbali nje ya
Jeshi. Hivi karibuni kumekuwa na mjadala juu ya uhalali wa uvaaji wa
sare hizo.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania linapenda kuwataarifu wananchi kuwa kulingana na kanuni za
Majeshi ya Ulinzi juzuu ya kwanza, viongozi hao wanaruhusiwa kisheria
kuvaa sare za Jeshi wanapokuwa wakitekeleza majukumu maalum, hivyo
wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi hao waliopo katika
maeneo yao.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
|
February 8, 2017
UFAFANUZI JUU YA UVAAJI WA SARE ZA JWTZ NA SHUKRANI KWA VYOMBO VYA HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment