Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa akitoa neno katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda Kapange iliyofanyika katika Hosppitali ya Taifa Muhimbili. |
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto wakishangilia huku wakiinua maua juu kama ishara ya upendo. |
Kushoto ni Mama Eda Kapange akikata keki katika hafla hiyo ya kumuaga, keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga |
Baadhi ya viongozi wakimtakia heri na afya njema mama Eda Kapange katika maisha yake baada ya kulitumikia taifa. |
Baadhi ya wauguzi na Madaktari wa
Idara ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika picha
ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.
……………………………………………………………………………..
Dar es salaam
Watumishi wa afya wamekumbushwa
kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya taaluma ya kazi ili
kuendelea kutoa huduma bora .
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar
es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili Agnes Mtawa alipokua akizungumza katika hafla fupi ya
kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda Kapange aliyekua akihudumu katika
katika Idara ya watoto.
Amesisitiza kuwa suala la
kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ni muhimu kwani mgonjwa anahitaji
upendo na kupewa maneno yenye matumaini na kwamba hiyo pekee ni tiba .
Pia Mkurugenzi Mtawa
amemuelezea Mama Eda Kapange kuwa ni mtumishi hodari na mchapakazi
hivyo amewataka watumishi wengine kuiga mfano wake kwa vitendo.
|
No comments:
Post a Comment